About us – Kiswahili

SISI NI NANI

GUTA TRADING (T) LTD inaagiza na kuuza Guta (Pikipiki ya Mzigo), Pikipiki na Spea kwenye chapa ya LIFAN. Kampuni imeanza biashara mwaka 2019 katika Mji mzuri wa Pwani wa Dar es Salaam, Tanzania.

Sisi tunaagiza na kuuza spea halisi ya LIFAN kwa sababu tunaamini kwenye ubora na bei inayokubalika kwenye soko ili wateja wetu wawe na amani wanapotumia bidhaa zetu kwa ajili ya matumizi ya binafsi au kibiashara.

Tulianza Biashara hii kwa sababu tuliona kuna mahitaji makubwa ya Guta (Pikipiki ya Mzigo) ambayo ni imara, zinadumu na ni rahisi kutumia na kutunza. Kwa hilo hatuna chaguo bora zaidi kuliko LIFAN.

LIFAN inajulikana sio tu hapa TANZANIA bali Duniani kote kwa ubora wake na uvumbuzi wake.

Ukifikiria Guta Fikiria Lifan

DHAMIRA YA KAMPUNI

Kuingiza na Kuuza Guta (Pikipiki ya Mzigo), Pikipiki na Spea za Guta na Pikipiki nchini Tanzania.

MAONI YA KAMPUNI

Kuwa Kampuni Inayoongoza na Kuaminika Nchini Kwenye Biashara ya Guta (Pikipiki ya Mzigo), Pikipiki na Spea za Guta na Pikipiki Tanzania.